September 29, 2015


Tayari Yanga wametua mjini Morogoro, mwenyeji wao naye amewakaribisha kwa kuwa yuko tayari kwa kazi ya keshokutwa Jumatano.


Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime ambaye wengine huchanganya na kumuita Mexime, amesema wako tayari kwa mechi hiyo ya Jumatano na Yanga wasitegemee mteremko.

Yanga wamekuwa na rekodi mbaya na Morogoro, kwa misimu miwili sasa wamekuwa wakipoteza mechi zao kwenye Uwanja wa Jamhuri dhidi ya Mtibwa Sugar.
Maxime amesema wao wako tayari, pia wanataka kuendeleza ushindi kama ilivyo kwa Yanga.

Yanga na Mtibwa zote zimeshinda mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu Bara na kila moja ina pointi 12.


“Kama ilivyo kwa mechi nyingine, tumejiandaa vilivyo. Waache waje tu wataona,” alisema Maxime ambaye kikosi chake tokea kuanza kwa msimu kimekuwa kikizigonga timu inazokutana nazo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic