September 21, 2015


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema uongozi wao sasa unataka kufanya vitendo zaidi ya maneno.


Sanga amesema anaamini Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri katika mechi yake ijayo dhidi yawatani wao Simba lakini sasa  ni vitendo zaidi.
“Kama ukisema maandalizi, naweza kusema tuko vizuri kabisa. Mwalimu na benchi la ufundi wamepewa kila walichohitaji.
“Kikubwa kwetu sasa ni mapambano na kufanya vitu kwa vitendo,” alisema.
Tayari Yanga imetia nanga kwa kuanza kambi yake kwenye visiwa vya Pemba kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Simba.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Yanga ililala kwa bao 1-0.

Yanga imekuwa ikihaha kurudisha heshima yake ya kuifunga Simba ambayo sasa inaonekana haina hofu hata kidogo kila inaposikia inakutana na Yanga.
Kwa mara ya kwanza msimu huu, timu hizo kongwe nchini zinakutana Jumamosi huku kila moja ikiwa imeshinda mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic