![]() |
| OKWI WAKATI AKIICHEZEA ETOILE DU SAHEL.... |
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limefungua kesi
kwenye Kamati ya Nidhamu ya FIFA dhidi ya klabu ya Etoile Sportive du Saleh ya
Tunisa kutokana na klabu hiyo kushindwa kuilipa klabu ya Simba SC ya Tanzania fedha za mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.
Kwa mujibu wa barua ya FIFA kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Tunisia (FTF) na nakala yake kwenda TFF, klabu hiyo inashitakiwa kwa
kuvunja kanuni kwa mujibu wa ibara ya 64 ya kanuni za nidhamu za FIFA (Fifa
Disciplinary Code).
Kwa
kuzingatia hilo, agenda hii itakuwa kwenye kikao kijacho cha kamati ya nidhamu.
Etoile
Sportive du Sahel wametakiwa kulipa mara moja kiasi cha dola za kimarekani laki
3 na riba ya asilimia 2% kwa kila mwaka kama ilivyoelekezwa na maamuzi ya Jaji
mmoja wa Kamati ya Nidhamu za Wachezaji mnamo tarehe 20 Novemba 2014.
Tangu
wakati huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekua likiwasiliana na
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tunisia (FTF) na FIFA kwa niaba ya klabu ya
Simba amabye ni mwanachama wa TFF.
Ikiwa
klabu hiyo ya Tunisia itafanya malipo kwa klabu ya Simba na kupelekea ushahidi
wa malipo kwa FIFA basi suala hilo litafutwa.
Aidha
klabu hiyo iko kwenye hatari ya kushushwa daraja au kupokwa alama kwenye
ligi (League Point) iwapo haitalishughulikia suala hilo mara moja.








0 COMMENTS:
Post a Comment