Kikosi cha Simba kimewasili
salama mjini Tanga kwa ajili ya mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.
Simba itafungua Ligi Kuu Bara kwa kuwa mgeni wa African Sports ‘Wana Kimanumanu’.
Nahodha wa Simba, Mussa
Hassan Mgosi amesema wamewasili salama na watafanya mazoezi mara moja.
“Tumefika Tanga salama,
tayari tuko kambini na tunasubiri maelekezo ya benchi la ufundi nini cha
kufanya,” alisema.
“Kuhusiana na mazoezi
tutafanya mara ngapi, ni suala la kocha na benchi lake la ufundi lakini
wachezaji tuko tayari kwa kweli,” alisema Mgosi.
Simba ilikuwa kambini mjini
Zanzibar na leo ilitumia usafiri wa ndege maalum kwenda Tanga ambako itaanza
ligi kwa kucheza mechi mbili dhidi ya African Sports, kabla ya kuivaa Mgambo,
Jumatano.
0 COMMENTS:
Post a Comment