September 4, 2015

MUSA AKIWA KATIKA MAZOEZI YA SUPER EAGLES KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR, LEO.
Mshambuliaji wa CSKA Moscow ya Russia, Ahmed Musa ni kati ya watu wa kuchungwa katika mechi kesho dhidi ya Taifa Stars jijini Dar es Salaam.


Katika mechi hizo tano, CSKA imefunga mabao 11. Musa ndiye mfungaji anayeongoza baada ya kupachika mabao matatu peke yake.
Usisahau Musa ni mzoefu na timu ya taifa ya Nigeria kwani alianzia U 20 halafu akapanda U 23 kabla ya kutua timu kubwa ya taifa.

Ingawa kazi yake kubwa ni kutengeneza mabao, katika mechi 50 alizoichezea Super Eagles, tayari ameishatupia mabao 10.

Ni mshambuliaji ambaye asipofunga, ana uwezo wa kusababisha mabao, hivyo lazima Stars pamoja na kucheza kitimu, basi wamtupie jicho la umakini mara mbili zaidi.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic