Pamoja
na kufanikiwa kuifunga Simba, mshambiliaji Amissi Tambwe amesema bado kikosi
chao kina kazi ngumu.
Tambwe
amesema kuifunga Simba hakuwezi kuwa majibu kwa Yanga kwamba sasa kila kitu
mbele yao ni lahisi.
“Katika
Ligi timu nyingi tu ni nzuri na haiwezi kuwa lahisi kwa kuwa ytumepata ushindi
basi kila kitu mbele yetu kitaenda kwa ulahisi.
“Wote
tunalijua hilo, tunaendelea kujituma ili tuendelee kufanya vizuri katika mechi
inayokuja dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema.
Tayari
kikosi cha Yanga kimetua mjini Morogoro kwa ajili ya mechi yake ya Ligi Kuu
Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mechi
yake ya mwisho, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba huku Tambwe
akifunga bao moja na kutoa pasi iliyosababisha bao la pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment