KOCHA MKUU WA NIGERIA, SUNDAY OLISEH AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI MARA BAADA YA KUTUA JIJINI DAR NA KIKOSI CHAKE. KUSHOTO NI MWANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI, WILBERT MOLANDI 'BABA ANDY'. |
Huku wakionyesha kuwa na umakini mkubwa,
maofisa wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) walikataa basi waliloandaliwa na
wenyeji wao, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakakodi lingine huku
wakimkataa dereva.
Maofisa hao pia waliwasili na vyakula
mbalimbali vikiwemo unga wa mahidi na mchele, maji, juisi na vifaa vingine vya
kupikia vyakula wakionyesha kuepuka hujuma wanazoweza kufanyiwa.
Wakiwa katika msafara wa watu 150 wakiwemo
wachezaji 23, uongozi wa Nigeria uligomea basi waliloandaliwa na TFF, wakaja na
yao mawili madogo pia wakakodi basi saizi ya kati aina ya Yutong linalofanya
safari kati ya Dar es Salaam na Moshi.
Hata hivyo dereva wa basi hilo ambaye hakutaka
kutaja jina lake aliliambia gazeti hili kwamba: “Wamekuja kulikodi Ubungo na
hawakusema kama watalitumia kwa timu ya taifa, nilipolileta wameniambia
hawahitaji dereva kwani wanaye wa kwao.”
Nigeria iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere kwa ndege binafsi na walitumia dakika 30 za ukaguzi kisha
msafara ukaondoka kuelekea Hoteli ya New Afrika na Hyatt Regency zilizopo
maeneo ya Posta.
0 COMMENTS:
Post a Comment