Azam
FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Ruvu JKT kwa mabao 4-2
kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Kwa
ushindi huo, Azam FC imefikisha 22 na kukwea kileleni siku ambayo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kupitia CCM
ametangazwa rasmi.
Mabao
ya Azam FC yamefungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Didier Kavumbagu Na
Kipre Tchetche wakati mawili ya JKT yalifungwa na Najim Magulu na Samwel
Kamuntu.
Mechi
ilikuwa kali, JKT ambayo sasa kocha wake wa muda ni Abdallah Kibadeni
ilionyesha soka safi lakini haikuwa makini katika ufungaji.
Achana na hivyo, safu yake ya ulinzi pia iliruhusu washambuliaji wa Azam FC kupenda na kufanikiwa kufunga kiulaini.
Hata
hivyo, Azam FC ilionekana kucheza kwa kujiamini zaidi ikipanga mashambulizi
kutokea nyuma na kufanikiwa kupata ushindi mnono.
0 COMMENTS:
Post a Comment