October 14, 2015



Uhuru Selemani amepania kufanya vizuri kweli, kwani wakati Ligi Daraja la Kwanza Afrika Kusini imesimama kwa muda, yeye ameendelea kujifua.


Ligi hiyo ilisimama kutokana na tarehe za Fifa kwa ajili ya kuwania kucheza Kombe la Dunia na kikosi chake cha Royal Eagles kikawa mapumzikoni.


Lakini Uhuru hakuacha kujifua kwa kuwa anajua wikiendi wana mechi dhidi ya Thanda Royal Zulu ambao wako fiti.

Tayari Uhuru ameishafunga mabao mawili na angependa kufunga zaidi.

“Kweli kulikuwa na mapumziko kidogo na ligi itaendelea wikiendi. Lakini niliendelea na mazoezi gym na uwanjani kwa juhudi kubwa.


“Nataka kufanya vizuri, ninajua mambo hayawezi kuwa lahisi,” alisema.


Uhuru amekuwa akifanya vema katika kikosi hicho amabcho anachezea kwa mkopo akitokea Jomo Cosmos ya Afrika Kusini pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic