Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameshtuka
na kubadili aina ya uchezaji katika mechi zote za Ligi Kuu Bara watakazozicheza
mikoani katika kuhakikisha wanapata ushindi. Yanga, leo Jumamosi inacheza dhidi
ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Yanga ina pointi 20 ikiwa haijafungwa mechi
hata moja lakini imeshinda sita na kutoka sare mbili, sare nyingine ya mabao
1-1 dhidi ya Azam FC. Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijm alisema ubovu
wa viwanja vya mikoani na wapinzani wao kucheza soka la kuwapania ndiyo tatizo
ambalo ameliona huku akitamba tayari amelipatia ufumbuzi.
Kwa kuanzia, Pluijm alisema ufumbuzi huo
utaanza kufanya kazi leo katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Kagera Sugar mjini
Tabora.
Pluijm alisema, kikubwa atakachokifanya ni
kucheza soka la mashambulizi ya kushtukiza na siyo kupiga pasi kutokana na
mazingira ya viwanja vya mikoani.
“Mfumo nitakaoutumia katika mechi tutakazocheza
Uwanja wa Taifa (Dar es Salaam) lazima utofautiane na ule ninaoutumiaga katika
michezo tutakayoicheza kwenye viwanja vya mikoani.
“Hivyo lazima nibadilishe mfumo kutoka wa
kucheza soka la pasi wakati tukiwa na mpira tunafanya mashambulizi kutokana na
ubora wa Uwanja wa Taifa tunaoutumia kama uwanja wetu wa nyumbani.
“Pia sitaki wachezaji wangu wagongane bila
sababu na wenzao wa timu pinzani kwani wanaweza kuumia bila sababu ya msingi,
hapa ni pasi ndefu tu,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment