Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel
mapema leo imezindua huduma ya ziada itakayowawezesha wateja wake kuangalia
vipindi vya televisheni mbalimbali katika vituo vya nje na ndani ya nchi
kwakutumia simu zao.
Akizungmza kwenye uzinduzi huo mapema
jana Makao Makuu ya Ofisi hizo, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando
alisema kwamba, kampuni hiyo imelazimika kuanzisha huduma hiyo yenye gharama
nafuu ili iweze kuwasaidia wateja wao kupata tarifa mbalimbali popote walipo.
“Airtel TV itawapatia fursa ya kipekee katika
kujihabarisha sehemu yoyote watakapokuwa kwa kutumia simu zao za mikononi,
kwani huduma hii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kutoa habari kirahisi,
mteja wetu ataweza kujiunga kwa bando la siku, wiki au mwenzi mzaiama”, alisema
Mmbando.
1: Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando, akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari (hawapo pichani), namna
watakavyoweza kujiunga na kufaidi habari kupitia huduma hiyo.
2: Mbando (kushoto), akizindua rasmi
huduma hiyo kwa kutumia simu yake ya mkononi huku Meneja wa huduma za ziada wa
kampuni hiyo Bi Prisca Tembo akishuhudia.
3:Mmbando akionyesha namna huduma
hiyo inavyopatika kwa urahisi katika simu mara tu baada ya kujiunga.
4: Meneja wa huduma za ziada wa
kampuni hiyo Prisca Tembo akifafanua zaidi namna unavyoweza kujiunga na huduma
hiyo bila usumbufu wowote ule.
0 COMMENTS:
Post a Comment