Beki wa pembeni wa Neckarsulmer, Emily Mgeta raia wa Tanzania
ameanza mazoezi mepesi kabla ya kurejea uwanjani.
Mgeta amekuwa majeruhi kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Neckarsulmer inayoshiriki daraja la tano
imemkukosa Mgeta baada ya kuumia mwezi uliopita.
Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka nchini Ujerumani,
beki huyo wa zamani wa Simba, amesema:
“Nimeanza mazoezi taratibu, lakini nimekuwa nikifanya
peke yangu. Baada ya hali kuimarika nitaungana na wenzangu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment