Kocha
Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema lazima Simba iongeze mshambuliaji ambaye
atakuwa ni tishio Tanzania.
Kerr
raia wa England amesema kuwa na mshambuliaji tishio ni sehemu ya uimara au
uhakika wa kikosi kufanya vema.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Kerr amesema kutaka mshambuliaji mkali zaidi haina
maana Simba haina washambuliaji wazuri.
“Lazima
uwe na kikosi kipana. Kuwa na kikosi kipana maana yake ushambuliaji, beki,
kiungo kote kunakuwa na chaguo kubwa.
“Najua
katika kipindi cha dirisha dogo nitashirikiana na uongozi kuhakikisha tunatatua
mapungufu kadhaa.
“Hili
si suala la Kerr au uongozi pekee. Hili ni suala la kila upande,” alisema Kerr.
Simba
bado haijawa na mwendo mzuri katika Ligi Kuu Bara ingawa hauwezi kusema ni
mwendo mbaya sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment