KOCHA MKUU WA KILIMANJARO STARS, ABDALLAH KIBADENI |
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo
alfajiri kikiwa na wachezaji 18 pamoja na vinogozi tayari kwa mashindano ya
Kombe la Chalenji yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.
Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha
mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa
katika kundi A, ikiwa na wenyeji timu ya taifa ya Ethiopia, Rwanda, pamoja na
Somalia.
Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni
magolikipa Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Kessy
Radmahani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ishaka, Salim Mbonde na Kelvin
Yondani.
Wengine ni viungo Himid Mao, Salum
Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya ushambuliaji
ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Saimon Msuva, Deus Kaseke na
nahodha John Bocco.
Stars itacheza mchezo wake wa kwanza
dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika uwanja wa Addis Ababa.
0 COMMENTS:
Post a Comment