Jose Mourinho ana bundi anamwandama. Maana Shirikisho
la Soka la England (FA) limemfungia kukaa kwenye benchi meshi ijayo dhidi ya Stoke
City na amelambwa faini ya pauni 40,000.
Ukiachana na mechi hiyo ya Premier League, Mourinho
ana presha kubwa kama atafeli katika mechi hiyo akiwa jukwaani, anatoa nafasi
ya Kocha Carlo Ancelotti na msaidizi wake, Claude Makelele kutua Stamford
Bridge kuchukua kazi yake.
Tayari imeelezwa Chelsea imefanya mazungumzo na wawili
hao na tayari wako mguu sawa, kutua Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment