Na Mwandishi Wetu, Johannesburg
Mshambuliaji
wa Stand United, Elius Maguli rasmi ametua jijini Johannesburg na kujiunga na
Taifa Stars.
Maguli
amejiunga na kikosi hicho chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa na kuanza
mazoezi.
Mara tu baada ya kujiunga na wenzake, Maguli alipewa dakika 45 tu za kupumzika kabla ya kuungana na wenzake mazoezini.
Maguli
alichelewa kujiunga na kikosi hicho baada ya kulazimika kubaki nchini aitumikie
Stars United iliyokuwa ikiivaa Mgambo.
Katika mechi
hiyo Maguli alifunga bao pekee lililoipa ushindi wa hiyo bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment