Michuano ya
Kombe la Shirikisho ya Azam Sports inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8,
2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Mechi rasmi
ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya
Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini
Musoma.
Siku hiyo pia
kutakuwa na mechi kati ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es
Salaam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Wenda
FC ya Mbeya na Madini SC ya Arusha.
Bingwa wa
michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania
kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Ratiba ya
raundi ya awali ya michuano hiyo imeambatanishwa (attached).
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment