November 3, 2015


Kocha wa Stand United, Patrick Liewig ameibuka na kusema sasa anataka nafasi ya tatu.


Liewig raia wa Ufaransa amesema ana imani na kikosi chake kwamba kinaweza kuchukua moja ya nafasi mbili za juu kama kila kitu kitakwenda kwa mpangilio.

Kocha huyo mkongwe raia wa Ufaransa, ameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa kikosi chake ambacho sasa kipo katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 19.

“Tunaweza kuwa moja ya timu mbili bora na tukafanikiwa,” alisema Liewig.
“Si lahisi kusema kila kitu kinawezekana kwa sasa, lakini mambo yanawezekana na kikubwa ni kuendelea kujifua,” alisisitiza.


Stand imekuwa ikionyesha mwendo mzuri chini ya kocha huyo raia wa Ufaransa ambaye aliwahi kuinoa Simba kabla ya kuondoka na kurejea kwao baada ya kutimuliwa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic