November 29, 2015


Nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kikosi chao bado kina nafasi ya kubadili mambo na kufanya vizuri na itawashangaza wengi.


Mgosi amesema licha ya kuwa na wachezaji wengi chipukizi, lakini Simba ina nafasi ya kufanya vizuri Ligi Kuu Bara itakapoanza Desemba 12.

“Unajua watu wengi hawajui kama Simba ina kikosi kizuri, imani yangu ni tofauti na wengi sana.

“Kikubwa watuamini na mashabiki na wanachama waungane nasi tupambane,” alisema.

Simba ilianza mazoezi ufukweni huku Kocha Dylan Kerr akiwakimbiza wachezaji kwelikweli.

Lakini sasa tayari imeingia katika programu ya kuutumia mpira zaidi.


Baada ya mechi 9, Simba iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic