N'DAW HEWANI |
Hatimaye sasa rasmi, klabu ya Simba imetangaza kuwatema
washambuliaji wake wawili wakigeni, Pape N’daw na Simon Sserunkuma.
N’daw raia wa Senegal ameonekana kama muigizaji na baada ya Kocha
Dylan Kerr kumpigia kura ya ndio kila mara, uongozi wa Simba umesema ndiye
aliyempendekeza aachwe.
Ndani ya mechi nane, N’daw hajafunga hata bao moja na ataendelea
kukumbukwa na lile tukio la kukutwa na hirizi maarufu kama Power Bank wakati
Simba ikicheza na Prisons.
Sserunkuma alisajiliwa msimu uliopita akitokea kwao Uganda, lakini
naye ameonyesha hakuna lolote.
SIMON SSERUNKUMA |
Wachezaji hao wa kigeni, walionekana hawana afaida yoyote katika kikosi cha Simba licha ya kuwa wakipata utetezi kutoka kwa benchi la ufundi, kwamba angalau wanaweza kuanza kung'ara na haikuwa hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment