Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo
hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF
zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana,
Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema
mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua
kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya
baadae.
Ole
Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi
hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo
wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo
wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.
Kikosi
hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho
alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini
ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya
kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi
(U17).
Baada
ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya
taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya
taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na
timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini
ya mkoa wa huo (U17).
Timu
inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza
michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani
Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
0 COMMENTS:
Post a Comment