December 23, 2015



Kampuni ya M-BET inayojishughulisha na michezo ya kubahatisha hapa nchini, juzi iliweza kuendeleza mapambano yake kupitia mchezo huo baada ya kumkabidhi zaidi ya shilingi milioni 17  Kiboko Isomba Samaki baada ya kubahatika kushindi moja ya mchezo wa kubahatisha unaoratibiwa na kampuni hiyo.

Tukio la kukabidhiwa kwa fedha hiyo limefanyika mapema hii kwenye ukumbi uliyopo katika Bar maarufu ya Samaki-samaki Masaki jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mbele ya wanahabari waliyojitokeza kushuhudia makabidhiano hayo katika Ukumbi uliyopo ndani ya  Bar maarufu ya Samaki-samaki Masaki jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba, alisema kwamba Kiboko Isomba kutoka kijiji cha Bulamba Bunda Mkoani Mara ni  mshindi wa pili kwa kujinyakulia kiasi kikubwa cha fedha kutoka M-BET.

“Nafarijika sana kumuona bwana Isomba akijinyakulia zaidi ya shilingi milioni 17, kwani inatia hamasa kwa watu wengine ambao wamekuwa hawana imani kubwa na michezo hii, kama mlivyomsikia mwenye amesema ametumia shilingi elfu moja tu na ndiyo imemfanya  kuondoka na milioni 17 huku akiifanya serikali kuchukua zaidi ya milioni 3 kama kodi kupitia michezo hii.

“Nitumie fursa hii pia kuwapongeza M-BET kupitia mkurugenzi wake Dhiresh Kaba, kwa kuendelea kutoa fursa ya watu kulipatia taifa kodi zake bila usumbufu kwani hapo awali baada ya Mwangasame kushinda milioni 28 aliiingizia serikali zaidi ya milioni 6 kama kodi kupitia michezo hiyo’, alisema Abbas Tarimba.

Kwa upande wa mshindi wa bahati nasibu hiyo Kiboko Isomba yeye amesema kwamba, anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kushinda fedha hizo kwani alikuwa na ndoto za kuja kushinda siku moja, japokuwa amekuwa akicheza mara kadhaa bila kubahatika hadi leo hii ambapo ametumia shilingi elfu moja na kubahatika kuopata milioni 17 tena kwa simu ya nokia ya tochi.

“Kweli kwenye maisha huwa hakuna matumaini yasiyokuwa na majibu sahihi, nasema hivi kwakuwa nimekuwa nikicheza michezo hii mara kadhaa bila ushindi lakini ijumaa ya Desemba 18 Mwaka huu ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwangua baada ya kupigiwa simu ikinifahamisha kuwa nimeibuka kuwa mshindi wa milioni 17 na leo hii nakabidhiwa.


“Fedha hii naimani itanisaidia kutatua ndoto zangu za kuendelea kuchukua digili ya pili katika chuo kikuu cha Makelele Uganda, ampako nilikuwa nikisoma mwanzo japo nilikuja  kukwama baada ya kuishiwa fedha za ada, mimi ni moja ya watanzania masikini na nimeshinda kutokea kijiji cha Bulamba Bunda mkoa wa Mara, hivyo nafarijika sana kutoka kote huko na kuja hapa kupokea hundi hii ambayo inaenda kuendeleza ndoto zangu,” alisema Kiboko Isomba Samaki.

Mshindi mwingine aliyewahi kubahatika na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 28 ni Robert Mwangasame wa kata ya Vwawa Mbozi Mkoani Mbeya ambaye kitaluma ni Mwalimu wa masomo ya hesabu katika shule ya Sekondari ya Vwawa.

   






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic