December 23, 2015


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Paul Nonga ameanza kazi baada ya kuifungia Yanga mabao mawili wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Yanga imeifunga Friends Rangers ya daraja la kwanza katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, leo.


Nonga amefunga mabao hayo mawili, moja akionyesha ana uwezo baada ya kumchambua na kumuacha beki Stephano Mwasyika na kuukwamisha mpira wavuni.

Bao moja lilifungwa na Thabani Kamusoko na Anthony Matheo.

Mshambuliaji huyo amejiunga na Yanga akitokea Mwadui FC katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Desemba 15.

Bao jingine la Yanga lilifungwa na Matheo Simon ambaye amejiunga na Yanga msimu huu.
Hata hivyo, Friends kutoka Magomeni Kagera ilitoa upinzani mkali hasa katika sehemu ya kiungo.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic