Azam FC imechoka kuishia hatua za awali
katika michuano ya klabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), sasa
imemwambia kocha wake ni lazima ahakikishe timu inafika hatua ya makundi msimu
ujao.
Timu hiyo ambayo ipo Tanga kwa mechi za
kirafiki, msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika linaloandaliwa na
Caf.
Tangu ilipoanza kucheza michuano ya
Caf, Azam haijawai kufika hatua ya makundi hivyo sasa uongozi umeamua kuweka
mikakati ya kuhakikisha inafika mbali msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor,
amesema kuwa, wamechoshwa kuishia hatua za awali za michuano ya Caf na sasa
wanataka kufika hatua ya makundi.
“Tumeshamwambia kocha (Stewart Hall)
moja kati ya masharti yetu kwake ni kuhakikisha tunafika kwenye makundi ya
michuano ya Caf kwani tumechoka kuishia hatua za awali.
“Tumejiandaa ipasavyo kuona
tunafanikiwa kufika mbali maana hapa kuna kazi ya kocha na nyingine ni sisi
viongozi,” alisema Idrissa.
Azam kwa sasa ipo Tanga ambako inacheza
mechi za kirafiki kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Desemba
12, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment