TP Mazembe ipo katika harakati za
kumuuza straika Mbwana Samatta kwenda Lille ya Ufaransa, lakini meneja wa
mchezaji huyo, Jamal Kasongo ametoa sharti jipya la nyota huyo kwa timu
atakayoenda.
Kirahisi tu, Kasongo amesema Samatta ni
lazima ajiunge na timu yenye uwezo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) au
Kombe la Europa, ambako anaweza kukutana na Wayne Rooney wa Manchester United
au Santi Cazorla wa Arsenal.
Kasongo alisema mpaka sasa wana ofa kutoka timu za mataifa matano lakini jambo
la msingi kwao ni kuangalia uwezekano wa kucheza katika klabu inayoshiriki
michuano mikubwa Ulaya.
“Bado tupo katika mazungumzo kwa sababu
ofa ambazo mpaka sasa tunazo mezani zinatoka katika nchi za Ujerumani,
Ufaransa, Bulgaria, Hispania na Ubelgiji, ila ukiitoa Bulgaria, nchi zilizobaki
anaweza kucheza.
“Hatuwezi kusema moja kwa moja kama
anakwenda Ufaransa kwa sababu tunataka timu ambayo itacheza michuano hiyo ya
Uefa na pia iliyo katika hali nzuri kwa masuala ya maslahi.
“Samatta akicheza Uefa au Europa
atakuwa amefika mbali sana na atajitangaza yeye mwenyewe na Tanzania kwa jumla
hivyo ni lazima tuliangalie hilo kwanza,” alisema Kasongo.
0 COMMENTS:
Post a Comment