Klabu ya Majimaji yenye makao yake makuu mjini Songea imefanikiwa kumsajili mshambuliaji
mkongwe nchini, Danny Mrwanda.
Mrwanda aliyewahi kukipiga na kung’ara akiwa Simba,
imeelezwa amesaini mkataba mfupi na Majimaji.
Kocha Msaidizi wa Majimaji, Hassan Banyayi amesema
Mrwanda amesajiliwa ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Kabla ya kwenda Majimaji alikuwa anakipiga Yanga
ambayo ilimsajili kutoka Polisi Moro.







0 COMMENTS:
Post a Comment