December 15, 2015

MGEVEKE (KATIKATI) AKIMDHIBITI ALIAS MAGURI KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA KATI YA STAND UNITED DHIDI YA MWADUI FC KWENYE UWANJA WA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA, JUZI. MWADUI FSC WALISHINDA KWA MABAO 2-0.

Na Saleh Ally
Unamkumbuka yule beki Joram Mgeveke, Simba walisema hakuwa ameiva sana, hivyo waliamua kumtoa kwa mkopo.

Kocha Jamhuri Kihwelo wa Mwadui FC akaamua kumtumia huku akisema anaamini hahitaji kusubiri na sasa ndiyo wakati wake.

Mgeveke amekuwa ndiye beki tegemeo kwa Julio na sasa anamtumia kama mmaliza ‘maasi’ kutoka kwa washambuliaji wa timu nyingine.

Ushahidi kama kweli Mgeveke chini ya Julio yuko vizuri ni katika mechi ya watani wa jadi mkoa wa Shinyanga, Stand United ambaoy walishinda kwa mabao 2-0.

Mgeveke ndiye alifanya kazi ya kumtuliza straika mwenye mabao mengi zaidi Tanzania Bara katika kipindi hiki, Elias Maguri.

Maguri ambaye ana mabao 9 katika Ligi Kuu Bara na moja timu ya taifa kwa msimu huu, alishindwa kufurukuta kwa beki huyo chipukizi aliyekuwa akitembea naye kila sehemu.

Hakika Julio amekuwa na uwezo wa kuona wachezaji wanaoonekana ni makinda na hawafai, akawapa nafasi na wakafanya vizuri.

Kocha huyo pua amekuwa na uwezo wa kuona wachezaji wanaoonekana ni 'wazee' au 'wamekwisha' lakini akawapa nafasi na wakafanya vema.

Kuna kila sababu ya kumpa sifa zake katika hilo hata kama atakuwa na kasoro zake katika soka, mfano maneno mengi, au kuna sehemu aliwahi kukwama. Lakini kwa upande huo kupitia hayo, amekuwa akifanya vizuri zaidi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic