Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewahi kuwa bonge la kipa hadi alidakia timu ya taifa ya Uholanzi.
Mara kadhaa, kocha huyo amekuwa akionyesha uwezo wake kwa kukaa langoni anapokuwa mazoezini Yanga.
Amekuwa akiwasaidia makipa Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ kuchukua ujuzi zaidi.
Kabla Yanga haijaondoka kwenda Tanga, mara kadhaa, Pluijm alionyesha ujuzi katika lango la Yanga akiwa mazoezi na kuwavutia mashabiki wengi waliojitokeza mazoezini.
Ingawa hakuwa akiruka kudaka, lakini alielekeza kwa ufundi mkubwa, namna gani kipa anaweza kukaa vizuri au kwa ufasaha langoni.







0 COMMENTS:
Post a Comment