Uganda ‘The Cranes’ wameibuka mabingwa
wa michuano ya Chalenji iliyomalizika leo nchini Ethiopia.
Bao la Uganda lilifungwa na Caesar Okhuti katika dakika ya 14 akiunganisha krosi safi kutoka Magharibi ya uwanja mjini Addis Ababa.
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilitolewa katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa kwa mikwaju 4-3 ya penalti na wenyeji Ethiopia ambao waling'olewa nusu fainali kwa penalti pia na Waganda.
The Cranes wameibuka na ubingwa baada
ya kuichapa Rwanda 'Amavubi' kwa bao 1-0.
Safu ya ilinzi ya Uganda ilikuwa
inaongozwa na beki wa Simba, Juuko Murishid ambaye ameingoza timu hiyo kubebwa
ubingwa dhidi ya Rwanda ambayo ilikuwa na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzoma na
kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza.
Licha ya Uganda kupata bao katika
kipindi cha kwanza, lakini mechi hiyo ilikuwa ya upinzani mkubwa hadi mwisho.
Uganda iliyoanza michuano hiyo kwa
kupoteza mechi kupoteza, inafundisha na Kocha Mserbia, Milutin Sredojevich ‘Micho’.
0 COMMENTS:
Post a Comment