Uongozi wa Mbeya City umekubaliana
kumpa mkataba wa miezi sita kipa Juma Kaseja ili aendelee kuitumikia timu hiyo.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya
Mbeya City kumpa mkataba aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo, Meja Mstaafu,
Abdul Mingange na kuwa kocha mkuu akiziba nafasi ya Juma Mwambusi aliyeenda
Yanga.
Mbeya City imeandaa mkataba huo mpya
kwa Kaseja kwani ule wa awali wa miezi sita tayari umeshaisha.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel
Kimbe, amesema: “Tumeridhika na kiwango cha Kaseja na hakuna kipa mbadala wake,
hivyo tunampa miezi sita mingine ili abaki.
“Tumeshaanza naye mazungumzo na nadhani
tutafikia makubaliano mazuri ili tuendelee kuwa naye kikosini, kwani pia ni
kiongozi anayefaa kwa vijana.”
Kimbe alisema tayari timu yake
imesajili wachezaji ambao ni Tumba Sued na Abdallah Juma huku mikakati ya
kuwanasa wengine ikiendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment