Mshambuliaji Paul
Kiongera ameungana na wenzake kambini mjini Zanzibar.
Kiongera raia
wa Kenya ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba, tayari “yuko
mzigoni”.
Taarifa za
uhakika zimeeleza Mkenya huyo aliyepelekwa kwa mkopo KCB, yuko kambini
Zanzibar.
Kutua kwa
Kiongera maana yake Simba imeongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji
ambayo ilikuwa inasua.
Mkenya huyo
aliichezea Simba mechi moja tu ya Ligi Kuu Bara ambayo ilikuwa ni ni dhidi ya
Coastal Union , bahati mbaya akaumia.
Simba ikaamua
kumuacha apate muda wa kupata matibabu na nafasi yake ikachukuliwa na wachezaji
wengine ambao hata hivyo walishindwa kuonyesha cheche.
0 COMMENTS:
Post a Comment