Kocha Mkuu wa Majimaji, Mika Lonnstrom, amefungashiwa kila kilicho chake rasmi na kisha mikoba yake ipo mbioni kuchukuliwa na kocha msaidizi wa timu hiyo, Hassan Banyai.
Mika aliondoka nchini Novemba 20, mwaka huu ambapo uongozi wa klabu hiyo umedai kuwa kuondoka kwake kumetokana na kibali chake cha kuishi, kuisha muda wake.
Chanzo kutoka Majimaji kimefunguka kuwa kocha huyo ameondoka nchini kutokana na kushindwana na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na malipo ya mshahara.
“Mike hataweza kurejea kuifundisha Majimaji kwani hii ni ligi ya Bongo na wanayoiweza ni Wabongo wenyewe, kuna mambo mengi yaliyochagia kuondoka kwa kocha, likiwemo hili la mshahara na si kweli kuwa kibali chake kimekwisha kama uongozi wanavyodai.
“Nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Banyai ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi kutokana na kuwa na Leseni B ambayo inamuwezesha kufundisha ligi kuu, pia ni kocha ambaye aliipandisha timu daraja, hivyo anafaa kuwa kocha mkuu,” kilisema chanzo.








0 COMMENTS:
Post a Comment