December 18, 2015


Straika mkongwe wa Simba, Mussa Mgosi, ameongeza familia baada ya Jumatatu ya wiki hii kupata mtoto wa kike.

Kwa maana hiyo, idadi ya watoto wake imeongezeka na kufikia watatu, kati ya hao mmoja wa kiume jina lake Hassani na wa kike ambaye ni Naylaty Mussa.

Mgosi amesema kwanza kabisa anajisikia faraja baada ya mke wake, Jasmine Elias kujifungua salama.

Mgosi alisema, mtoto huyo mpya amepewa jina la Nayfaty, hiyo ni baada ya mabishano ya muda kati ya dada na kaka wa mdogo wao huyo ambao kila mmoja alipendekeza jina la kumpa mdogo wao.

“Mabishano ya dada na kaka wa mtoto mpya yalikuwa makubwa sana kutokana na kila mmoja kupendekeza jina lake analoona linamfaa.


“Vita ilikuwa kubwa sana lakini mwisho wa siku jina la dada mtu ambalo ni Nayfaty ndiyo likapita, hivyo hilo jina tulilompa atakuwa akiitwa,”alisema Mgosi ambaye hajaongozana na timu yake kwenda Mwanza kucheza dhidi ya Toto, kesho Jumamosi. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic