December 3, 2015




Na Saleh Ally
Nawakumbusha tu wale wapenda michezo wanaopenda kuwazeesha wachezaji baada ya kitu kidogo tu kutokea.

Abdi Kassim ‘Babi’ au Michael Ballack wa Unguja alionekana ni ‘Mzee’ na hajiwezi.

Lakini leo zaidi ya mwaka wa pili anaendelea kuitumikia timu yake ya UiTM ya Malaysia na anafanya vizuri. Ingawa sasa yuko rikizo kwao Zanzibar, lakini ni mtu ambaye unaweza kusema amethubutu na anastahili sifa.

Babi ambaye ni mtaratibu ndiye nahodha wa timu hiyo ambayo ina wachezaji watatu tu kutoka Afrika.

 

Ukiona hata picha anazopiga na kutupia mtandaoni anaonyesha ni mtu mwenye furaha kubwa kubwa.

Huenda kupitia Babi tunaweza kujifunza mambo mengi sana. Kuanzia kwa wachezaji kwamba hawatakiwi kukata tamaa.

Maana Babi angekata tamaa, Azam FC ingekuwa ni mwisho wake. Hakukubali ameondoka na hata kama hachezi ligi kubwa, lakini anacheza soka na anaishi kwa kuingiza kipato huenda kuliko ambacho angepata Tanzania.

Mabadiliko ya maisha yanataka ujasiri. Babi ameonyesha na wachezaji wengine wafuate hasa wale ambao wamekata tamaa umri ukiwa bado unawaruhusu.

Kwa mashabiki, pia wanapaswa kuachana na tabia ya kuwazeesha na kuwakatisha tamaa wachezaji wengi wa Kitanzania kwa sababu ya chuki binafsi au kubahatisha mambo.

Watanzania wengi wameacha kucheza soka au wamekata tamaa wakati wana uwezo. Wameacha hivyo kwa kuwa tu wamekatishwa tamaa na wao wakakubali kusimamishwa na kushindwa kuendeleza ndoto zao.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic