Hadi sasa kikosi bora cha Premier League kinaonekana kuwa hicho unachkiona.
Lakini mambo yanaonekana kuwa si mazuri kwa vigogo
wengi na wachezaji wengi wa timu vigogo.
Utaona Chelsea haina mchezaji hata mmoja wakati
ilikuwa ikitawala kikosi hicho kwa miaka sita sasa.
Vigogo wengine Liverpool na Manchester United nao
walewale, hawana mchezaji wakati timu kama Leicester City imeingiza wachezaji wawili
katika first eleven ambao ni Jamie Vardy na Riyad Mahrez.
Arsenal inaonekana kuwa bomba kabisa kwani nayo
imeingiza wachezaji wawili ambao ni kipa mkongwe Petr Cech na kiungo nyota Mesut
Ozil.
Everton nayo ina wachezaji wawili ambao ni
washambuliaji Romelu Lukaku na Ross Barkley.









0 COMMENTS:
Post a Comment