December 23, 2015

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans der Pluijm anajua mshambuliaji wake, Donald Ngoma ni msumbufu na kumthibiti inataka ufundi na juhudi kubwa.

Kutokana na hali hiyo, Pluijm ameamua kumpa kazi beki Vicent Bossou amthibiti Ngoma katika mazoezi ya Yanga.

Katika kila mazoezi ya Yanga, kama itakuwa ni kupambana beki na mshambuliaji, basi Bossou raia wa Togo amekuwa akipewa kazi ya kumkaba Ngoma.

Pluijm ameamua kufanya hivyo ili kumuimarisha Bossou ambaye alitua nchini akiwa ‘legelege’ na kulazimika kumtupa benchi.

Kutokana na kuhenyeshwa na Ngoma mara kwa mara akianguka kama mzigo, inaonyesha angalau kumpandisha Bossou kiwango na anaweza kuendelea kupata nafasi ya kikosi cha kwanza Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic