December 2, 2015

RAIS ABDEL AZIZ
Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz ametoa kali ya mwaka baada ya kulazimisha mechi iishe katika dakika
  ya 63 na kutaka timu zipigiane mikwaju ya penalti.

Rais huyo alionekana kukerwa na uchezaji wa taratibu katika mechi ya Super Cup iliyokuwa inazikutanisha timu za FC Teyragh-Zeina na ACS Ksar na tayari zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mwamuzi alifikishiwa ujumbe huo ambao ulitoka kwa rais aliyekuwa jukwaani. Naye hakuwa na ujanja zaidi ya kutimiza hilo, mikwaju ya penalti ikapigwa.
Hata hivyo, suala hilo lilikuwa gumzo na kusababisha tafrani baadhi ya mashabiki wa soka wa Mauritania wakilaani uamuzi huo wa rais wa nchi yao kuingilia masuala ya soka.

Baada ya hapo, Ikulu ya Mauritania ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikanusha rais huyo kuhusika na suala hilo huku ikisisitiza ni uzushi mtupu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic