Wachezaji wa Yanga wametoa kali ya mwaka baada ya kufanya kazi ya wahudumu wa huduma ya kwanza kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Yanga ilikuwa ikipambana na African Sports, wakati dakika zinayoyoma wachezaji wa Sports walionekana kupoteza muda kwa makusudi, wengine wakijiangusha.
Wakati daktari alipoingia kuwahudumia naye alifanya mambo taratibu ndipo Thabani Kamusoko, Vicent Bossou na Deo Munish ‘Dida’ wakaamua kufanya kazi ya kumbeba mchezaji aliyeumia.
Kilichoutia ni kasi yao ya kumpeleka mgonjwa nje ya uwanja, hali ambayo imezua gumzo kwamba ukicheza na Yanga, Red Cross wapumzike tu!
Hapa kazi tu
ReplyDelete