Yanga na Azam FC zitawajua wapinzani wao kwenye michuano ya kimataifa soon maana wanatarajiwa kuwekwa hadharani Desemba 15, mwaka
huu tayari kwa kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la
Shirikisho Afrika.
Yanga inaiwakilisha Tanzania kwenye
michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu msimu
uliopita, huku Azam yenyewe ikiiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la
Shirikisho.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, ameeleza kuwa kufuatia ratiba hiyo inayotarajia
kutoka Desemba 15, Yanga imeandaa mikakati madhubuti kuhakikisha inafanya vyema
katika michuano hiyo.
“Ratiba ya Caf itakuwa hadharani ifikapo
Desemba 15 na sisi kama Yanga tayari tuna mikakati yetu tuliyoiandaa kuelekea
michuano hiyo ili kuweza kufanya vyema.
“Tupo katika mazungumzo na timu tano kwa
ajili ya kucheza nazo mechi za kirafiki ili kuimarisha timu yetu kuelekea
michuano hiyo ambapo miongoni mwa timu hizo zinatoka nchi za Afrika Magharibi.
“Tutatumia michuano ya FA na Kombe la
Mapinduzi kwa ajili ya kuwaangalia wachezaji wa kikosi cha pili huku wale wa
kikosi cha kwanza wakitumika kujiandaa na michuano ya Caf kwa kucheza mechi
hizo,” alisema Tiboroha.
Ubingwa wa michuano hiyo unashikiliwa na
TP Mazembe na Yanga wanataka kutumia mechi hizo tano kwa ajili ya kuwavua
ubingwa huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment