December 11, 2015

Uongozi wa Yanga umempongeza mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kwa kufanikiwa kupata tuzo ya Mjasiriamali Kijana Afrika kupitia Kampuni yake ya Quality Group Limited kuwa ni moja ya mafanikio na wao kama klabu wanajivunia kupitia mwenyekiti wao na wamemuandikia barua ya kumpa hongera.


Manji amefanikiwa kupata tuzo hiyo ambayo alikabidhiwa nchini Mauritius baada ya kusaidia mapambano ya Ugonjwa wa Ebola ambao uliozikumba nchi za Afrika baada ya kutambuliwa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni.

 Katibu wa klabu hiyo, Dk Jonas Tiboroha amesema kuwa kiongozi wao ni mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio hayo, hivyo anastahili pongezi kwa mafanikio hayo.

“Ni jambo la kujivunia kama klabu kwa sababu ni mafanikio na sisi kama viongozi tumemuandikia barua kiongozi wetu ya kumpongeza kwa sababu si jambo dogo na hii ni kutokana na juhudi zake katika kazi yake na kuweza kufikia mafanikio hayo.


“Kiukweli tunampongeza kwa kuwa anaitangaza klabu yetu kwa sababu katika kazi yake na CV anafahamika kama mwenyekiti wetu, pale anapofanya vema na klabu inafaidika, hasa katika kujitangaza, hivyo anastahili pongezi,” alisema Tiboroha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic