January 15, 2016


Siku chache baada ya Klabu ya Simba kumtimua kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, imejulikana wazi kuwa Muingereza huyo hana mpango wa kuondoka Tanzania hivi karibuni.

Awali, Kerr alinukuliwa akisema anasubiri malipo yake ya kuvunjiwa mkataba wake kisha aondoke nchini lakini baadaye akabadili msimamo na kusema kuwa hana mpango wa kuondoka nchini haraka.

“Hata kama atalipwa nahisi ataendelea kubaki kwa madai kuwa ameyazoea mazingira ya Bongo, hivyo anataka kuvuta muda zaidi wa kukaa,” alisema mtu wa ndani wa Simba na kuongeza:


Kerr alipoulizwa juu ya malipo yake na kuhusu kuondoka, alisema: “Labda leo (jana) ndiyo watanilipa lakini pia sina mpango wa kuondoka haraka, nafikiri naweza kwenda visiwani Zanzibar kupumzika kwa muda.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic