January 22, 2016

FRIENDS RANGERS
Uongozi wa klabu ya Friends Rangers, umesema klabu ya Yanga isitarajie mteremko katika mchezo wao wa kutania Kombe la  FA, utakaofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ofisa habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, amesema licha ya kujua wanacheza na timu inayoongoza Ligi Kuu, wao wamejipanga kushinda mchezo huo.

"Kikosi chetu kipo kambini na kila kitu kinakwenda vizuri kabisa kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya Jumapili.

"Kikubwa nilitaka kuwatahadharisha Yanga, wasitarajie mteremko eti kwa kuwa wanakuja kucheza na Friends Rangers. Tuko vizuri na tutawashangaza," alisema Kigundula akionyesha imani kubwa na kikosi chake.

Kigundula alisema Yanga isiifananishe timu yao na timu iliyoifunga mabao 5-0, hivyo kwao wanakuja kamili kuhakikisha wanaitoa na kuendelea katika hatua inayoufuata.

"Tumejipanga kushinda hivyo Yanga ifute ndoto za kutufunga kwa sababu juzi ilipata ushindi wa mabao mengi, wameifunga timu ambayo ilipanda kizengwe wasubili waone tutakachowafanya"alisema Kigundula

Hata hivyo Kigundula amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi katika mchezo wao ili waweze kuwapa hali zaidi wachezaji wao wacheze kwa kujiamini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic