January 22, 2016

KOCHA MINGANGE NA BAADHI YA WACHEZAJI WA MBEYA CITY

Baadhi ya mashabiki wa Mbeya City wamemtaka kocha mkuu wa timu hiyo Meja Mstaafu Abdul Mingange,  pamoja na uongozi kuachia ngazi kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo inayapata.

Tangu Mbeya City ilipoanza kuwa chini ya Mingange imeshinda michezo miwili, imefungwa michezo minne, sare nne.

Kutokana na matokeo hayo mashabiki wengi wamekuwa wakionyesha kuwa na hasira dhidi ya viongozi.

Wakizungumza na Championi kwa nyakati tofauti mashabiki hao walilalama kuwa matokeo hayo yakiendelea hivyo, basi kuna uwezekano mkubwa wa timu kushuka daraja, hivyo ni bora hatua zikachukuliwa mapema.


Upande wa uongozi wa Mbeya City kupitia kwa katibu mkuu, Emmanuel Kimbe, alisema watakaa na benchi la ufundi kujua tatizo na kuwataka mashabiki kutulia. 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic