January 22, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limejitoa katika sakata la aliyekuwa nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ likisema kuwa suala hilo anahusika nalo kocha mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa.

Cannavaro alitangaza kustaafu kuichezea Stars wiki moja iliyopita baada ya kufanya mahojiano na gazeti la Championi na blogu ya SALEHJEMBE.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa alisema suala hilo hawatakiwi kuliingilia na badala yake wamemuachia kocha mwenyewe.

“Tunashangaa suala hilo kuchukuliwa kubwa na kukuzwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na isitoshe wakati Cannavaro anapewa unahodha hakupewa barua zaidi ya kuonekana akivaa kitambaa uwanjani.


“Pia maamuzi ya kuichezea au kutoichezea Stars tumemuachia kocha mwenyewe anayeona mchezaji yupi anafaa kuichezea Stars,” alisema Mwesigwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic