Kocha Mkuu wa muda wa Simba, Jackson Mayanja amewataka makipa Peter Manyika na Vicent Agbani raia wa Ivory Coast kuwa katika utimamu wa asilimia mia kwa fitnesi.
Mayanja raia wa Uganda amewataka makipa hao kuongeza mazoezi kuhakikisha wanakuwa walinzi sahihi katika kila dakika 90 za mechi.
“Kwa mchezaji wakati wote anatakiwa kuwa fiti kwa asilimia mia, kipa ni mlinzi namba moja. Akipitiwa yeye, maana yake mmefungwa, hivyo anatakiwa kuwa fiti kamilifu.
“Mchezaji anapokuwa timilifu kwa maana ya kuwa fiti sana, basi uhakika wa kufanya anachotaka iwe ni kwenye kuokoa au kushambulia unakuwa juu sana. Hivyo nimewasisitiza na wao wanalijua hilo,” alisema.
MAYANJA (KULIA) AKIWA MAZOEZINI NA KIKOSI CHA SIMBA... |
Kwa sasa Simba haina kocha wa makipa baada ya Iddi Salim raia wa Kenya kutupiwa virago na uongozi wa Simba na tayari ameisharejea kwao Nairobi, Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment