February 27, 2016


Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amepanga kumtumia beki wake Pato Ngonyani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Sababu ni moja tu ya kumtumia Pato leo, kwamba alicheza vizuri dhidi ya Simba wikiendi iliyopita akiwa kiungo namba sita na kuiwezesha Yanga kushinda mabao 2-0 katika Ligi Kuu Bara.


Katika kuonyesha amenogewa na kazi ya Pato, katika mazoezi ya jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, Pluijm alionekana akimuelekeza vitu vingi kwenye nafasi ya kiungo namba sita.


Pato alikuwa na kazi moja tu katika mchezo huo, kutibua mipira yote ya viungo wa Simba iliyokuwa ikitengenezwa kwenda kwa washambuliaji na hawakuweza kufurukuta.
Hiyo ina maana kwamba, Pato atacheza mbele ya mabeki wa kati wawili kati ya Kelvin Yondani, Vincent Bossou au Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye amerejea uwanjani kutoka majeruhi. 


Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Yanga, amesema: “Kocha amepanga kumtumia Pato kucheza namba sita kwenye mechi ya kesho (leo) baada ya kuvutiwa naye alipocheza dhidi ya Simba.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic