February 27, 2016



Simba ilipata kona nane katika mchezo wake dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita, lakini haikuweza kunufaika na hata mojawapo kwani zote zilipigwa kwa mtindo mmoja tu.

Sasa Yanga imebaini tatizo hilo la Simba, kwani imeshafanyia kazi aina tofauti za kupiga kona kuelekea mchezo wake wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.


Simba licha ya kupata kona hizo, ilijikuta ikiambulia kipigo cha mabao 2-0 yaliyofungwa na Donald Ngoma na Amissi Tambwe ikiwa ni ushindi wa pili kwa Yanga dhidi ya timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu Bara.


Katika mazoezi yake ya jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, alionekana akiwaelekeza wachezaji wake namna ya kupiga kona hizo.


Wapigaji wakubwa wa kona hizo walikuwa ni Simon Msuva na Deus Kaseke na walipiga zile ndefu za kuelekea golini kwa adui na nyingine fupi za kutengeneza mpira pembeni ya lango.


Katika mazoezi hayo, Msuva alionekana kufanya vizuri katika kona alizopiga kwa maelekezo ya Pluijm katika muda wote wa mazoezi hayo ya asubuhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic