February 14, 2016


Unaweza kusema Mungu si wa mmoja. Kwani baada ya presha kubwa, hatimaye Valencia imeshinda mechi ya kwanza chini ya Kocha Mkuu Garry Neville na msaidizi wake, Phil Neville ambaye ni mdogo wa kocha mkuu.

Valencia ikiwa nyumbani imeichapa Espanyol kwa mabao 2-1 na kuwapa akina Neville ahueni baada ya presha kubwa huku wakifukuzwa na mashabiki wa Valencia.

Mabeki hao wa zamani wa Man United sasa watakuwa na nafuu baada ya ushindi huo wa kwanza wa La Liga ingawa wanatakiwa kuuendeleza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic