February 1, 2016

KAMUSOKO

Timu ya Yanga, juzi Jumapili ilichezea kichapo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu, ilipochapwa mabao 2-0 na Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Coastal, Ally Jangalu, amesema kuwa, aliyeimaliza Yanga katika mechi hiyo ni kiungo wao wa kimataifa, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

Alisema katika mechi hiyo, Yanga walikuwa wakimtegemea zaidi Kamusoko kuwatengenezea nafasi za kufunga washambuliaji wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma ambao kwa pamoja mpaka sasa wameshafunga mabao 22. Tambwe ameshazifumania nyavu mara 13 wakati Ngoma tayari ameshatupia wavuni mabao tisa.

“Baada ya mimi kugundua hilo, ilibidi nimwekee mtu ambaye atavuruga kabisa hesabu zake, jambo ambalo lilifanikiwa, kwani kila alipokuwa akishika mpira, kijana wangu huyo (Ayoub Semtawa) alifika na kumtibulia.

“Pia nilikuwa nimempatia majukumu ya kuituliza timu pindi tunaposhambuliwa lakini pia kuanzisha mashambulizi ya kasi pale tunapokuwa na mpira, hakika jukumu hilo alilitekeleza kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kumpoteza vilivyo Kamusoko,” alisema Jangulu ambaye amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akichukua mikoba ya Jackson Mayanja ambaye sasa anainoa Simba.

Baada ya ushindi huo, Coastal Union ilipanda juu katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 14 iliyokuwa ikishika hapo awali, mpaka ya 11 ikiwa na pointi 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic