February 6, 2016



Beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy kwa sasa anaonekana kuwa na kiwango cha juu zaidi kuliko washindani wake wawili.

Washindani wakubwa wa Kessy kwa nafasi hiyo ni Juma Abdul wa Yanga na Shomari Kapombe wa Azam FC ambao kwa michezo mitatu ya ligi iliyopita, Kessy anaonekana kuwa juu.

Kapombe hajashiriki mechi mbili za ligi kwa kuwa Azam FC ilisafiri kwenda Zambia katika michuano maalum.

Wakati Juma Abdul ambaye anarejea kutoka majeraha bado hajaonyesha kiwango cha juu.

Kessy pamoja na kufunga bao, lakini amekuwa akichangia utengenezaji wa mabao.

Kasi yake, ubunifu pia unafanya awe kama winga au mshambuliaji hatari anayeogopwa na mabeki wengine.


Hata hivyo, bado Kessy atakuwa na upinzani mkali kwa kuwa Kapombe ambaye ni beki anaongoza kwa kufunga mabao na Abdul, ni mabeki wenye kasi, nguvu na wanaojituma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic